Ruka hadi maudhui kuu

Kuwa msajili

Mahitaji ya uidhinishaji, nyaraka zinazohitajika, na jinsi ya kuwasilisha maombi yako.

Taasisi zinazotaka kuwa wasajili walioidhinishwa zinahitaji:

  1. (a)kuomba Mamlaka kwa kujaza fomu ya maombi katika Ratiba ya Kwanza ukurasa wa 10 wa kanuni.
  2. (b)kulipa ada za uidhinishaji na utawala zilizoainishwa katika Ratiba ya Pili ya Kanuni hizi.
  3. (c)Maombi yanakamilishwa kupitia portal ya Tanzanite.

Nyaraka zifuatazo lazima ziambatane na maombi ya uidhinishaji:

  1. (a)wasifu wa biashara;
  2. (b)nakili iliyothibitishwa ya cheti cha usajili wa kampuni; au
  3. (c)uthibitisho wa uidhinishaji wa ICANN; na
  4. (d)nyaraka nyingine yoyote kama Mamlaka itakavyoelekeza.

Baada ya kupitia maombi yaliyotumwa, Mamlaka inaweza kuidhinisha muombaji kama msajili aliyeidhinishwa.

Ikiwa muombaji hajazingatia mahitaji ya maombi yaliyoainishwa katika kanuni hii, Mamlaka inaweza kukataa maombi au kuomba marekebisho madogo.

Taarifa za kina zinapatikana katika kanuni hii.